28 Julai 2026 - 12:40
Iraq Yapokea Zaidi ya Mazuwwari Milioni 1.8 kwa Ajili ya Ziara ya Arbaeen ya Imam Hussein (a.s)

Zaidi ya mahujaji milioni 1.813 wameingia Iraq tangu mwanzo wa mwezi wa Muharram. Mahujaji hao wametoka katika mataifa 172 duniani kushiriki Ziara ya Arbaeen ya Imam Husayn (a.s). Mamlaka za Iraq zimesema maandalizi ya kiusalama na huduma kwa mahujaji yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) –ABNA– Iraq imetangaza kuwa zaidi ya mahujaji milioni 1.813 kutoka mataifa 172 tofauti wameingia nchini humo tangu kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Muharram kwa lengo la kushiriki Ziara ya Arbaeen ya Imam Husayn (a.s).

Mkuu wa Kitengo cha Habari za Usalama nchini Iraq, Luteni Jenerali Saad Maan, amesema kuwa hadi sasa jumla ya mahujaji 1,813,000 wamewasili nchini Iraq, huku idadi hiyo ikiendelea kuongezeka kadiri siku za kuelekea Arbaeen zinavyosogea.

Ameeleza kuwa serikali ya Iraq, kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na taasisi mbalimbali za huduma, imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha mahujaji wanapata ulinzi, usafiri, huduma za afya na mazingira salama katika safari yao ya kuelekea miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.

Ziara ya Arbaeen ya Imam Husayn (a.s) ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani, ikiwakusanya mamilioni ya waumini kutoka pembe mbalimbali za dunia kila mwaka kwa ajili ya kuadhimisha siku ya arobaini tangu kuuawa shahidi kwa Imam Husayn (a.s) katika tukio la Karbala.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha